17th June, 2020
Huenda hazina ya kitaifa inayosimamia masuala ya maji
Ikakosa ufadhili iwapo wahisani kama ubalozi wa denmark,
Ubalozi wa uswidi na benki ya ujerumani zitajiondoa
Kutokana na fununu za uvunjaji sheria katika uongozi wake.
Hii ni baada ya kubainika kuwa afisa mkuu mtendaji wa
Halmashauri hiyo ismael fahmy shaiye anapania kujiongezea
Kipindi cha tatu cha kuhudumu kinyume na sheria.
Mwanahabari wetu lofty matambo anatathmini jinsi mamlaka
Mbali mbali serikalini zilivyo kiuka agizo la mkuu wa utumishi
Wa umma joseph kinyua na kusalia na maafisa kwa kipindi
Kirefu ama kuwaajiri maafisa wasiofaa kisheria.