12th June, 2020
Jamii ya talai katika kaunti ya nandi imesisitiza kwa mara
nyingine kuwa haiwezi kumpa baraka mtu mwingine haswa
naibu rais william ruto ikizingatiwa kuwa ilimuidhinisha rais
uhuru kenyatta na kumpa mavazi ya kiongozi kwa mujibu wa
tamaduni za jamii hiyo. Mzee wa jamii hiyo christopher koyugi
amesema kuwa waliomfanyia naibu rais sherehe hiyo
walikiuka kaida zilizowekwa na viongozi wote
hawakuhusishwa. Naibu rais william ruto alikuwa huko wiki
iliyopita akitaka baraka za kugombea urais katika uchaguzi
mkuu wa 2022