12th June, 2020
Hali ya taharuki ilitanda nyumbani kwa mwanamziki wa nyimbo
za ohangla marehemu benard onyango baada ya mamia ya
waombolezaji kukabiliana na maafisa wa
polisi.maafisa wa polisi
walilazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya maelfu
waliojitokeza kushuhudia usafirishaji wa maiti ya marehemu
kutoka hospitali ya port florence ambako mwili wa
marehemu ulikuwa umehifadhiwa hadi nyumbani
kwake.msongamano mkubwa ulishuhudiwa na kuathiri
shughuli ya kuusafirisha mwili huo.iliwabidi polisi kubadili
njia mara kadhaa ila juhudi zao ziliambulia
patupu.waombolezaji waliwazuia maafisa hao wakitaka mwili
wa marehemu kuhifadhiwa hadi kesho kwa kigezo cha mila na
tamaduni kisha wakaweka mchanga kwenye kaburi ili
asizikwe.polisi walichimba tena kaburi hilo ila waombolezaji
waliuchukua mwili wa marehemu na kutoroka nao.jeneza la
marehemu liliharibiwa wakati wa vuta nikuvute hiyo.