28th May, 2020
Polisi wa kituo cha Kahawa West hapa jijini Nairobi wanalaumiwa kwa kumpiga jamaa mmoja na kumjeruhi vibaya wakati wa kafyu. Jamaa huyo kwa jina Samuel Maina anadai alikumbana na polisi hao wakati wa kuwafukuza watu kwenda manyumbani, akapigwa nusura afariki.