8th March, 2020
Huku ulimwengu ukisherehekea siku ya kina mama, mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Uasin Gishu hana cha kujivunia wala kusherehekea. Milicent Chepkurui ambaye huishi na mwanawe wa kike mwenye umri wa miaka ishirini na minne ambaye hana uwezo wa kutembea na upande wake wa kushoto kupooza, wanaishi tu kwa kudra za mwenyezi Mungu kutokana na changamoto anazozipitia.