.
22nd January, 2020
Mgogoro wa uongozi katika chuo kikuu cha Nairobi unazidi kutokota huku professa Stephen Kiama ambaye uteuzi wake ulifutiliwa mbali na waziri wa elimu George Magoha na baadaye kurejeshwa na mahakama akiapa kuendelea kutekeleza majukumu yake ya naibu chanzela wa chuo hicho. Mgogoro huo umeibua hisia mseto chuoni hapo huku uongozi wa wanafunzi wa chuo hicho na muungano wa wahadhiri na wafanyikazi wakisema hawamtambui kiama kama mkuu wa chuo hicho.