.
30th December, 2019
Familia moja huko Molo kaunti ya Nakuru inaomboleza kifo cha mwana wao ambaye aliuawa na mumewe. Lucy Waithera mwenye umri wa miaka 35 ameripotiwa kukatwa na panga shingoni na mumewe hapo jana, kwenye kile kinachosemekana kuwa ugomvi wa nyumbani. Mwanamume huyo kwa jina Joseph Ngigi anasemekana alimkata shingo mkewe, mbele ya mtoto wao wa umri wa miaka mitatu. Mshukiwa alitoroka na sasa anasakwa na polisi.