1st April, 2019
Genge moja hatari limeibuka mtaani Kayole ambalo linawahangaisha wakazi. Usiku wa kuamkia leo, mfanyabiashara mmoja alivamiwa na kuuawa na genge hilo kwa kudungwa visu mara kadhaa, jambo ambalo sasa limezua hofu. Asasi za usalama zinaombwa kulivalia njuga suala hilo.