25th February, 2019
Kaunti ya Mandera imetoa ufadhili wa elimu kupitia mpango wa kaunti kuleta mabadiliko ya elimu kwa wanafunzi wake. Kupitia mpango huo wa kipindi cha mwaka huu, Gavana wa Kaunti ya Mandera Ali Roba, ametenga milioni 126 kuwasaidia wanafunzi bora wanaotoka katika familia masikini.