.
11th February, 2019
Hatimaye familia moja mjini Nakuru imepata fursa ya kuzika mwili wa baba yao aliyefariki miezi nane iliyopita. Hii imewezekana baada ya hospitali ya Nakuru war memorial kusalimu amri na kuachilia mwili wa marehemu elvis mwaura. Mwili huo ulikuwa umezuiliwa baada ya familia ya marehemu kushindwa kulipa deni la shilingi milioni mbili na nusu ambayo ni gharama ya matibabu na ada ya kuhifadhia maiti.