.
28th November, 2018
Afisa mkuu mtendaji wa nhif, Geoffrey Mwangi na mkurugenzi wa fedha, Wilbert Kurgat, wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au pesa taslimu nusu milioni. Hakimu mkuu, Francis Andayi, aliwaagiza wawili hao wawasilishe stakabadhi zao za usafiri mahakamani. Kuachiliwa kwa wawili hao kulitokea saa chache tu baada ya bodi ya shirika la nhif kuwasimamisha kazi kwa muda.