.
26th November, 2018
Sekta ya uzalishaji maziwa katika Kaunti ya Kisii imeimarika kwa kasi katika kipindi cha miaka 4 sasa kufuatia kuzinduliwa kwa teknolojia ya uhimilishaji (artificial insemination) kwa bei nafuu na kuwepo kwa wataalum kwa karibu. Teknolojia hiyo inaonekana kupunguza kurudiarudia upandikizaji wa ng’ombe na kuwapunguzia gharama wafugaji. Kiwango cha maziwa katika kaunti hiyo kimeimarika huku wakulima wakisema kuwa ni kwasababu ya mbegu bora zilizopandikizwa kwa ng,ombe.