15th October, 2018
Mwanahabari wa runinga ya citizen, Jacque Maribe na mpenzi wake, Joseph Irungu almaarufu jowie, leo walikana mashtaka ya mauaji ya mfanyibiashara monicah kimani na kuzuiliwa tena rumande hadi siku ya jumatano ambapo ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana litasikilizwa na kuamuliwa. Wakati huo huo jaji wa mahakama kuu jessy lesit aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ametangaza kujiondoa.