8th October, 2018
Viongozi wa kaunti ya Lamu wameungana na kuunga mkono mradi wa kawi ya upepo katika wadi ya bahari eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu wakizungumza katika mkutano na wakulima wa eneo lililoathirika na mradi huo viongozi hao wamewafahamisha wakulima kuhusu mfumo wa kuwalipa ridhaa unaojulikana kama rap utakaotumiwa na muekezeji kwa minajli ya kujua ni mfumo upi wa malipo wanaotaka waathiriwa wa mradi huo. Mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama amewaonya wanaotaka kutia doa zoezi hilo. Muthama aidha amesema watakaofaidika na ridhaa hiyo ni wakulima halali wa eneo hilo pekee.