3rd October, 2018
Police huko Bureti katika kaunti ya Kericho wamemkata mwanamume mmoja aliyemuua mwanawe alipokataa kwenda shuleni. Inadaiwa kuwa David Malel alichukua fimbo na kumpiga kijana wake ambaye alifia hospitalini wakati madaktari walipokuwa wakijaribu kuyaokoa maisha yake. OCPD wa Bureti Mohammed Ali amesema kuwa walimkamata mshukiwa katika eneo la Kapkatet.