29th September, 2018
Siku ya afya ya moyo duniani imesherehekewa leo na katika eneo la Magharibi mwa Kenya sherehe hizo zilifanyika katika kaunti ya vihiga ambapo kituo cha kwanza cha kupima na kutibu maradhi ya moyo kimeanzishwa katika hospitali ya rufaa ya vihiga. Maradhi ya moyo yamejumuishwa miongoni mwa yale yanayochangia vifo vya ghafla kimataifa.