.
23rd September, 2018
Maafisa nchini Tanzania wamesema kuwa idadi ya watu waliofariki katika mkasa wa feri ya MV Nyerere iliyozama katika ziwa Victoria Alhamisi iliyopita imefikia watu 224 huku miili zaidi ikitarajiwa kuokolewa kutoka katika feri hiyo.
Waziri wa ujenzi, uchukuzi pamoja na mawasiliano Isack Kamwelwe amesema miili zaidi huenda ikapatikana katika operesheni inayoendelea.
Jamaa za waliofariki wameanza kutambua miili ya wapendwa wao katika kisiwa kidogo cha ukara ambako mkasa huo ulitokea.