.
10th July, 2018
Serikali imeshikilia kwamba kamwe haitawafidia wakazi wa Kibera watakaoathirika na ujenzi wa barabara inayojengwa kupitia mtaani humo. Naibu wa mwenyekiti wa tume ya ardhi, Abigael Mbagaya, amesema ardhi ya kibera ni mali ya serikali hivyo hapatakuwapo na fidia yoyote ila msaada tu wa kuwasaidia watakaoathirika. Naye mwenyekiti wa tume ya taifa ya haki za binadamu, Kagwiria Mbogori, amesema ingawa ni lazima haki ya kila mkenya izingatiwe, fidia italenga tu kuwasaida waathiriwa kuendelea na maisha bila ya faida yoyote ya ziada.