2nd July, 2018
Mkutano wa wabunge wa Jubilee uliotarajiwa kufanya hapo kesho umeahirisha. Duru zikiarifu kuwa chama kinapanga kuandaa mkutano wa faragha nje ya jiji la nairobi kwenye harakati za kuziba nyufa ambazo zimedaiwa kuibuka chamani. Hata hivyo katibu mkuu wa chama cha jubilee raphael tuju amekanusha kupangwa kuwepo kwa mkutano wowote hapo kesho.