.
14th June, 2018
Raia waliojawa na hasira wamemvamia na kumpiga hadi kufa mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo katika eneo la Car Wash mjini kisumu kwa madai kuwa alihusika katika kifo cha msichana mmoja ndani ya nyumba yake. Inadaiwa mshukiwa huyo alikuwa akijaribu kutoroka baada ya kumuua msichana huyo na kupakia mwili wake ndani ya begi.