12th March, 2018
Jamii zinazoishi kando ya misitu zitapewa miche ya kupanda ili kusaidia kurejesha uzito misitu nchini ambayo inaendelea kuharibiwa. Hii ni kauli yake waziri wa mazingira Keriako Tobiko aliyekuwa akizungumza baada ya kuzuru misitu ya Oloolua, Ngong, Kibiku na Thogoto iliyoko kanti za Nairobi na Kiambu. Tobiko alielezea wasiwasi wake kufuatia visa vya uharibifu na jinsi wanabiashara wa kukata miti wanavyokubaliwa kufanya biashara bila kutarajiwa kupanda miche kujaza nafasi iliyokatwa.