30th January, 2018
Kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha Karua amejiunga na wakili wake Gitobu Imanyara katika kesi inayopinga ushindi wa gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru. Imanayara akiwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya rufaa mjini Nakuru amesema atashirikiana na Karua katika rufaa hiyo. Karua aliketi kando ya mawakili wengine akiwa na mavazi rasmi ya mahakamani.