.
23rd January, 2018
Mchezo wa kuvivinjari umegeuka karaha katika mabonde ya Kerio baada ya waruka parachuti wawili – raia wa kigeni kuanguka na kufariki papo hapo. Watalii hao ambao ni mkufunzi na mwanafunzi walikuwa wakiruka kwenye parachuki moja kabla ya kupoteza uthibiti na kuanguka kwenye bonde. Tukio hili limejiri majuma mawili baada ya raia mwingine wa kigeni kufariki katika bonde hilo. Mkuu wa polisi Keiyo North mwenda meme amesema wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.