26th November, 2016
Aliyekuwa rais wa zamani wa Cuba, Fidel Castro amefariki. Fedel Castro alifariki hapo jana usiku na viongozi mbalimbali wanazidi kutoa salamu za rambirambi kwa raiya wa nchi hiyo ambao waliumuenzi Castro kwa siku nyingi. Katika utawala wake Castrol alitofautiana pakubwa na marekani iliyodhania kuwa alikuwa akiendeleza uongozi wa kiimla. Alikuwa uongozini kwa kipindi cha zaidi ya miaka 40 baada ya kuipindua serikali ya Cuba mwaka wa 1959 na kuifanya nchi ya kikoministi. Miongoni mwa waliotuma risala zao nchini ni kiongozi wa ODM Raila Odinga hali kadhalika katibu mkuu wa vyama vya wafanyikazi nchini Francis Atwoli