×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

KTN Leo: Maafisa watatu na raia mmoja wafiskishwa mahakamani kwa kuiba petroli huko Nakuru, 16/11/16

16th November, 2016

Maafisa watatu wa polisi na raia mmoja wamefikishwa katika mahakama ya Nakuru kwa tuhuma za kuiba bidhaa za mafuta ya petroli inayogharimu shilingi milioni 8.6. Fredrick Omondi, Justus Mutinda, Kelvin Nzai na Evans Kamau wanadaiwa kushiriki wizi huu kati ya tarehe 8 na tarehe 10 mwezi huu wa Novemba katika eneo la Sobea kaunti ndogo ya Rongai kaunti ya Nakuru. Yadaiwa wanne hao walishirikiana na wengine ambao hawakuwa mahakamani.  Bidhaa hiyo ya petroli inadaiwa kuwa sehemu ya ushahidi katika kesi iliyo mahakamani inayomhusu Evans Kamau anayetuhumiwa kwa kuuza bidhaa za petroli kinyume cha sheria.  Wanne hao hata hivyo walikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa bondi ya shilingi nusu milioni kila mmoja na milioni moja pesa taslimu. 

.
RELATED VIDEOS