.
27th October, 2016
Shirika la action aid hivi leo limezindua mchango wa kutafuta fedha za kujenga hifadhi ya wasichana wanaokwepa ukeketaji wa wanawake eneo la west Pokot. Hifadhi hiyo itagharimu kima cha shilingi milioni 14 ikidhamiriwa kukisaidia kikundi cha kina mama cha KOMESI, kaunti ya west Pokot. Hafla hiyo ilihudhuriwa na miongoni mwa viongozi wengine, mkewe gavana wa west Pokot, bi Josephine Kachapin na wakuu wa shirika la action aid. waweza kuchangia hifadhi hiyo kupitia nambari ya 889610 jina la akaunti.