5th October, 2016
Vita vya maneno kati ya naibu wa rais William Ruto na mwanaharakati Boniface Mwangi vinaonekana kuchukua mkondo tofauti. Hii ni baada ya naibu wa rais kutishia kumpeleka mahakamani, huku mwanaharakati huyo kupitia wakili wake Gitobu Imanyara, akimwandikia barua ya kujibu.