.
19th September, 2016
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema kwamba kuondoka kwa baadhi ya wanachama waliohamia chama cha Jubilee hakuwababaishi. Kalonzo amewataka wahusika kufuata sheria na kung’atuka rasmi ili maeneo wanayowakilisha yafanywe chaguzi ndogo. Aidha amesema angali kwenye kinyang’anyiro cha urais ndani ya muungano wa CORD.