.
25th August, 2016
Kikosi cha Kenya cha mchezo wa Tong Il Moo Do kinapania kutetea taji lake pale mashindano ya kimataifa yatakapong’oa nanga siku ya jumamosi katika ukumbi wa shule ya Aga Khan mjini Mombasa. Ingawa timu hiyo imekuwa mazoezini kwa muda wa wiki mbili pekee, katibu mkuu wa shirikisho la mchezo huo nchini Hillary Wahanda ana imani kuwa wana uwezo wa kushamiri.