×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mwanamke mhalifu atiwa mbaroni mjini Nyeri baada ya kupatikana na bastola

11th August, 2016

Kizaazaa kiliibuka katika kituo cha basi mjini Nyeri baada ya mwanamke mmoja kukamatwa na polisi akiwa na bunduki aina ya pistol ndani ya mkoba wake. Mwanamke huyo aliyeonekana kuwa na mimba alikuwa ameandamana na mwanamume mwingine ambaye wenyeji wa Nyeri wanadai kuwa aliachiliwa kutoka jela mwaka jana. Wawili hao walikuwa wameabiri matatu ya kutoka Nyeri kuelekea nanyuki lakini kabla ya gari hilo kuanza safari, maafisa wa polisi walifika na kuwaamuru wawili hao kutoka nje ya gari. Mwanamke huyo alijaribu kuurusha mkoba huo chini ya kiti lakini akagunduliwa. Hapo ndipo polisi waliukagua mkoba wa mama huyo uliokuwa na bunduki ndani pamoja na pakiti moja ya taulo za hedhi. OCPD wa Nyeri Makua Mutua amesema kuwa watawachunguza zaidi iwapo mwanamke huyo ni mja mzito au la au hata iwapo hutumia hali yake kuwahada watu na kuwaibia. Wawili hao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Nyeri.

.
RELATED VIDEOS