Wakuu wa chama cha ODM wapuuza utafiti wa IPSOS
3rd August, 2016
Chama cha ODM sasa kinapania kuwasilisha mswada bungeni ili kuyadhibiti mashirika ya kiutafiti nchini. ODM kupitia kaimu katibu mkuu agness zani wameonekana kughadhabishwa na matokeo ya utafiti wa hivi punde uliofanywa na shirika la ipos synovate wakiyapuuzilia mbali. ODM inashikilia msimamo kuwa kanuni na mfumo haukufuatwa.