Hilary Clinton ateuliwa rasmi na chama cha democratic kuwa mpeperushaji wa bendera
27th July, 2016
Bi Hilary Clinton sasa ameteuliwa rasmi na chama cha democratic kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama hicho kwenye kinyang’anyiro cha mwezi Novemba nchini marekani. Bi Clinton ametajwa kuwa mgombeaji rasmi kwenye kongamano la chama hicho linaloendelea jijini Philadelphia jimbo la Virginia nchini marekani. Mwanahabari wetu Alex Chamwada anahudhuria kongamano hilo na sasa anaarifu kuhusu ufanisi huo wa Bi Clinton na kipute hicho kwa ujumla