Familia ya binti wa chuo kikuu cha Kenyatta aliye uawa yadai haki
27th July, 2016
Familia ya msichana aliyeuawa na mpenzi wake mtaa wa kahawa kaunti ya Kiambu imefutilia mbali madai kuwa mwanamme aliyemuua alikuwa akimlipia karo katika chuo kikuu cha Kenyatta alikomaliza masomo yake. Baba ya marehemu msichana huyo anasema ndiye aliyemlipia karo binti yake kwa usaidizi wa mikopo ya wanafunzi HELB.