Sonko atoa msimamo wake kwa muungano wa Cord
23rd July, 2016
Seneta wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko amesema kuwa atahama muungano wa Jubilee endapo Cord itamteua Kalonzo Musyoka kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao. . Alikuwa akizungumza katika mazishi ya babake mbunge wa Mavoko Patrick Makau Kaloleni kaunti ya Machakos. Wakuu wa cord Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka walikuwepo