×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Ababu akinzana vikali na viongozi wa ODM kuhusu viongozi wanaotuhumiwa kueneza matamshi ya chuki

3rd July, 2016

Huku kiongozi wa CORD Raila Odinga akiwaongoza wakuu wa CORD kutangaza kwamba muungano huo utawatetea viongozi wake wanaotuhumiwa matamshi ya uchochezi, katibu mkuu wa chama cha ODM Ababu Namwamba amekuwa katika hafla ya maombi katika kaunti ya Busia ambapo amekosoa mwenendo wa wanasiasa kutoa matamshi ya chuki. Ababu amesema kwamba yeyote anayetoa matamshi ya chuki anafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali misingi ya vyama. Ababu ameonekana kukinzana vikali na viongozi wake huko Machakos ambao wasema kwamba watasimama kidete na viongozi wao wanaotuhumiwa kueneza matamshi ya chuki. Aidha Kalonzo, Raila na Wetangula wamesema kwamba serikali ya Jubilee inatumia swala la matamshi ya uchochezi kuukandamiza upinzani. Viongozi hao wanapanga kuzuru eneo la Suna kumkaribisha Junet Mohamed kwao akiwa mmoja kati ya sita waliokuwa rumande Pangani na kujipatia jina ‘ the Pangani six’.
.
RELATED VIDEOS