Waziri mkuu Cameron atarajiwa kujiuzulu baada ya Uingereza kujiondoa katika muungano wa ulaya
25th June, 2016
Waziri mkuu wa uingereza David Cameron anatarajiwa kujiuzulu kabla ya oktoba mwaka huu baada ya nchi hiyo kupiga kura ya kujiondoa katika muungano wa ulaya. Akizungumza baada ya matokeo kutangazwa, Cameron amesema kuwa hataweza kuongoza meli inaoyoonekana kuzama. Baadhi ya athari za moja kwa moja za uamuzi huo ni pauni ya Uingereza kushuka dhidi ya dola kwa mara ya kwanza tangu 1985.