×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Saleh Wanjala 'James Bond wa Bungoma' afikishwa kortini

18th May, 2016

Mwanamume aliyedandia ndege iliyokuwa imeubeba mwili wa mfanyi biashara aliyeuawa Jacob Juma mnamo siku ya Ijumaa iliyopita, hatimaye amefikishwa katika mahakama moja mjini Bungoma na kushtakiwa na kosa hilo. Jamaa huyo Saleh Wanjala aliyebandikwa jina la kimajazi James Bond wa Bungoma, alifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kuhatarisha maisha yake na ya walioabiri helikopta hiyo. Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu wa Bungoma Stephen Onsiero Mogute. Hakimu huyo aliamuru kuwa Saleh Wanjala, aachiliwe kwa dhamana ya bure ya polisi, hadi siku ya Ijumaa wiki hii, huku polisi vilevile wakipewa muda wa kutathmini ni kiwango kipi cha dhamana ambacho jamaa huyo atatakikana kulipa mbele ya mahakama. Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Western Kenya Human Rights Watch limepinga vikali kushtakiwa kwa Saleh Wanjala, huku mkurugenzi wake Job Bwonya akipendekeza kushtakiwa kwa afisa mkuu wa polisi wa Bungoma Kusini, na hata rubani wa ndege hiyo, kwa kile alichokitaja
.
RELATED VIDEOS