x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Hofu ya kuzuka kwa maradhi ya Kipindupindu imetanda katika shule ya upili ya wavulana ya Narok

11, May 2016

Hofu ya kuzuka maradhi ya Kipindupindu imetanda katika shule ya upili ya wavulana ya Narok baada ya zaidi ya wanafunzi 40 kufikishwa hospitalini wakiwa na dalili za kutapika na kuendesha . Baadhi ya wanafunzi walilalamikia kuumwa na tumbo. Hata hivyo mwalimu mkuu wa shule hiyo amefutilia mbali madai kuwa huenda wamekula chakula kichafu. Watabibu wangali wanachunguza ugonjwa huo. Wanafunzi 814 , walimu na wafanyikazi 200 wa shule hiyo wamepokea dawa za kuangamiza viini vya kipindupindu.Maafisa wa afya pia wanachunguza hali ya usafi wa maji yanayotumika shuleni humo.

RELATED VIDEOS


Feedback