Vurumai katika Bunge la kaunti ya Mombasa baada ya wawakilishi wa wadi kutofautiana
11th May, 2016
Vurumai imezuka Alasiri ya leo kwa siku ya pili katika Bunge la kaunti ya Mombasa baada ya wawakilishi wa wadi kutofautiana kuhusu kuendelea kwa vikao bungeni. Mgogoro huu ambao ulianza hapo jana ulipalilia rabsha ya aina yake pale wanahabari walipohujumiwa na kuzuiliwa kuingia bungeni kunakili matukio hayo. Spika Thaddeus Rajwayi alionekana kushindwa kuthibiti hali hiyo iliyochukua takriban saa mbili cheche za matusi na vishindo vikishamiri