Wilson Kipsang' atarajia kuwakilisha Kenya katika mbio za olimpiki huko Rio
5th May, 2016
Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya marathon wa hapo awali Wilson Kipsang amedokeza kuwa angependa kuwakilisha Kenya kwenye michezo ya olimpiki Rio licha ya kutokuwa katika nafasi ya tatu bora katika mbio za marathon za London mwezi uliopita.kipsang alitwaa nishani ya shaba kwenye michezo ya olimpiki ya makala ya 2012 jijini London.