x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Gor Mahia yalaza Bandari, Ulinzi yasajili ushindi dhidi ya Chemilil Sugar

28, Apr 2016

Gor Mahia imeendeleza msururu wake wa matokeo mema katika ligi kuu nchini baada ya kulaza Bandari 2-0 katika mechi ya ligi kuu nchini huku kikosi cha Ulinzi kikisajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Chemilil Sugar. John Makwata alikuwa wa kwanza kucheka na wavu katika dakika ya 32 hii ikiwa ni kabla ya Hillary Echesa kuwasawazishia Chemilil Sugar. Bao la pili na la ushindi kwa ulinzi likawa ni lake John Makwata kupitia kwa penalty. Katika mechi tofauti, bandari ilikosa kumakinika na kupata kichapo cha 2-0 huku George Odhimba akifunga la kwanza naye Felly Mulumba akajifunga na kumaliza mechi 2-0. Sonny sugar ikalaza kakamega Homeboyz 1-0 Posta Rangers nayo ikatwaa alama tatu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ushuru na mechi ya Tusker dhidi ya Mathare United ikakamilika 2-2

Feedback