Mashindano ya riadha ya idara ya wanajeshi
27th April, 2016
Hellen Obiri alirejea mashindanoni kwa kishindo licha ya kuwa katika likizo ya misimu miwili. Bingwa huyo wa zamani wa mbio za dunia ndani ya uwanja alinyakua taji la mbio za mita elfu tano katika mashindano ya riadha ya idara ya wanajeshi katika uga wa Kasarani mapema hii leo.