Viongozi watoa rambirambi zao kwa rais mustaafu Mwai Kibaki kwa kumpoteza mkewe Lucy Kibaki
26th April, 2016
Rais mustaafu Daniel arap Moi, ametoa rambirambi zake kwa familia ya rais mustaafu Mwai Kibaki kwa kumpoteza Mama Lucy Kibaki. Kwenye taarifa rasmi rais Moi ameomboleza kifo cha mama Lucy akisema ni pigo kubwa kwa taifa na familia ya Kibaki. Amemwomba mola kuipa familia ya Kibaki nguvu wakati huu mgumu.