Wachuuzi wahatarisha maisha yao kuendeleza biashara zao ya uchuuzi barabarani
25th April, 2016
Kila uchao, swala la uchuuzi linazidi kukithiri katika kaunti ya Nakuru na viungani mwake huku idadi yake ikiendelea kukua. Katika barabara kuu ya Nakuru - Eldoret kuna wachuuzi ambao licha ya kuhatarisha maisha yao wanaendeleza biashara zao bila kujali.