Msongamano mrefu wa magari yatatiza shughuli za usafiri katika barabara ya kutoka Mombasa - Nairobi
25th April, 2016
Shughuli za usafiri katika barabara ya kutoka Mombasa - Nairobi sehemu ya kaunti ya Machakos zilisimama kwa takriban saa kumi kuanzia usiku wa kuamkia leo. Kulishuhudiwa msongamano mrefu uliotokana na ajali,na kuwalazimisha baadhi ya wasafiri kulala barabarani. Pia kuna madai ya mgomo unaoendelezwa na madereva wa magari ya masafa marefu.