Vinara wa CORD Moses Wetangula, Kalonzo Musyoka na Raila Odinga wafurushwa kwa vitoa machozi
25th April, 2016
Vinara wa CORD Moses Wetangula, Kalonzo Musyoka na Raila Odinga walifurushwa kwa vitoa machozi baada ya kuivamia afisi za IEBC wakitaka kuwang’atua kwa nguvu makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC. Wafuasi wa CORD walijaribu kutumia mabavu kuvunja lango kuu la kuingia jumba la Anniversary na kuwalazimu polisi kuwatimua.