Msimamo wa COTU: amewataka waajiri kote nchini kuwaongezea mishahara wafanyikazi wao
24th April, 2016
Muungano wa Vyama vya Wafanyikazi nchini COTU umefanya mkutano wake wa maombi kwa matayarisho ya kusherehekea siku ya wafanyikazi duniani jumapili ijayo. Katibu Mkuu wa muugano huo Francis Atwoli amewataka waajiri kote nchini kuwaongezea mishahara wafanyikazi wao na kuboresha maisha yao kutokana na uchumi wa Kenya kupanda. Naye kiongozi wa CORD Raila Odinga amesema serikali yaJubilee inastahili kufanya juhudi za kuwaunganisha Wakenya kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.