Naibu RUTO awataka CORD kukoma kuwahadaa Wakenya
23rd April, 2016
Kwengineko Naibu rais William Ruto amewataka wakuu wa CORD kukoma kuwahadaa wakenya kuwa taasisi huru nchini zinaweza kuvunjwa bila kuzingatia sheria. Ruto amekosoa mapendekezo ya CORD na baadhi ya wanasiasa kutaka tume huru ya uchaguzi na mipaka kuvunjiliwa mbali kabla ya uchaguzi mkuu ujao.