Kiongozi wa vijana wa chama cha ODM jijini Nairobi Stephen Mukabana auawa
13th April, 2016
Wafuasi wa ODM jijini Nairobi wanaomboleza kifo cha kiongozi wa vijana wa chama jijini katika Stephen Mukabana. Mukabana ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mihango. Polisi katika eneo la Njiru hapa Nairobi wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo.