Gavana Oparanya amkosoa Wetangula kwa kuitaka jamii ya Waluhya kujiunga na Ford Kenya
11th April, 2016
Muungano wa CORD unakabiliwa na tatizo kubwa la kuamua atakayegombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kati ya Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula. Wafuasi wa vigogo hao wanazidi kuwapigia debe wakuu wao huku Wetangula akisema yeye ndiye bora zaidi. Kadhalika naibu kiongozi wa ODM Wycleffe Oparanya amemkosoa Wetangula ambaye anaitaka jamii ya Waluhya kujiunga na Ford Kenya.